Menu
 

Mkali wa miondoko ya RnB na Dancehall Bongo Belle 9 ambaye kwa sasa anatamba na Ngoma ya Mfalme, amedai yeye yupo tofauti na wasanii wengine wanaochora Tatoo kwenye miili yake, kwani hafikirii kufanya hivyo licha yakupenda mitindo.


"Sijafikiria kuchora Tattoo lakini nadhani kwa vile nimezungukwa na marafiki ambao wamechora tattoo,kwa hiyo nikijiona sina tattoo najiona niko tofauti hicho ndio kinachonifanya ni-delay kuchora Tattoo" amesema Belle 9 kupitia kipindi cha The Splash cha Redio Ebony FM.

Hata hivyo ameeleza Tattoo kamili na yenye kitofauti anayojivunia iliyopo kwenye mwili wake. "By the way nina original tattoo kwenye mikono yangu ambayo niya meno, off course ninayo tu sitaki kusema ilikuaje ha ha ha haaaaa(lakini awali alisema ni ya kung'atwa na mwanamke)".

Endelea kufurahia muziki mzuri kutoka kwa Belle 9 kupitia ngoma yake hii mpya iitwayo Mfalame. 

Post a Comment

 
Top