Menu
 


Kwa muda wa wiki mbili, kumekuwepo na tetesi zilizozagaa kuhusu Msanii anaetokea Yamoto Band, Maromboso kuhusishwa kuwa amemwaga wino na kuwa miongoni mwa wasanii waliopo kwenye Music Label ya Wasafi/WCB.

Msanii Maromboso wa Yamoto Band.
Lakini tetesi hizo zimezidi kuonaga zaidi baada ya Msanii huyo pia kuonekana katika Video ya kutangaza biashara mpya ya Karanga iitwayo DiamondKaranga bidhaa wa Msanii na Rais wa WCB Diamond Platnumz.

Meneja wa WCB Sallam Sk Mendez amezifungukia kiundani tetesi hizo kupitia Kipindi cha The Splash kinachosikika kupitia Redio Ebony FM.

Meneja wa WCB Sallam Sk.
Chochote kinawezekana kwa sababu Maromboso ni Msanii mzuri na ana uwezo na yuko Yamoto yuko Mkubwa na Wanae na Mkubwa na Wanae meneja wao ambae ni Mkubwa Fella ni party ya Board  Directors wa WCB so chochote kinawezekana na hakuna kinachoshindikana kwa sababu mzunguko ni ule ule” amesema Sallam Sk.

Post a Comment

 
Top