Menu
 

Baada ya kuenea kwa tetesi Nchini Nigeria toka mwaka 2016 kuwa Koko Master D 'Banj kamuoa kwa siri Lineo Didi Kilgrow sasa imekuwa si siri au tetesi na sasa taarifa zimekuwa wazi.


D'Banj amethibitisha rasmi katika interview na Beat FM ya Nigeria kuwa kamuoa mwanamke mrembo Lineo toka mwaka jana baada yakuona yafaa kuchukua uamuzi huo na amekuwa mwenye furaha na maisha toka alivyooa.

“Nilimuoa Didi kwa siri kwa sababu na ufahamu kuhusu umuhimu wakufanya jambo hilo muhimu katika maisha kwa siri kwa sababu ni jambo langu binafsi, mahusiano ya namna hii ni ya amani na furaha kuliko kuyatangaza hadharani kwa sababu kuna watu ambao maisha yao wameyaelekeza katika kukosoa na kukatishana tamaa nikaepukana nao ili nilibadili uamuzi wa kuoa" amesema D'Banj huku akiwa mwenye bashasha tela.

Hitmaker huyo wa Emergency amechukua uamuzi huo wa kuthibitisha kuoa baada ya kubahatika kupata mtoto mmoja wa kiume na amedai maisha yake yamekuwa na bahati kubwa baada ya kuoa mwanamke mwenye sifa zote za kuitwa mke bora.

Post a Comment

 
Top