Menu
 


“Hivi ama Vile” ni ngoma ambayo imelenga pande mbili za maisha ya kila siku zenye upinzani wa jadi, na imefanikiwa kuingia mjini vema na kuteka hisia za mashabiki wa muziki mzuri wa kundi la HipHop liitwalo Rostam linaloundwa na Wasanii wawili Roma na Stamina.

Crew Mamber wa Rostam, Stamina amepigia Mstari katika kipindi cha The Splash cha Redio Ebony FM na kuipa tafsiri matata ya ngoma hiyo wakati akihojiwa na Watangazaji Chris Bee na Fredoo Mbunji.


“Kila mtu ana kitu chake ambacho anakipenda na anachokipenda mwengine inabidi mwingine ukiheshimu, na sometimes kuna mwingine anaweza asikipenda sana hicho kitu lakini kwa sababu umekipinga naye akamaamua kutafuta kitu kingine kinachofanana ili akipinge” amesema Stamina.


Wakati huo tukiendelea kuburudika na ngoma hiyo, Stamina ameweka bayana mikakati ya kundi hilo la Rostam yakujiweka karibu zaidi na mashabiki wao ikiwa ni pamoja na suala la Albamu. 


Hii Ngoma haitokuwa kwenye Albamu yangu, itakuwa kwenye albamu ya Rostam ambayo tunaitarajia kuitoa very soon hii ndio nyimbo ya kwanza ya Rostam, tunachoomba tu ni support tunatarajia kuleta nyimbo nyingi”Amenukuliwa Stamina.

Post a Comment

 
Top