Menu
 


Rapper na Muanzilishi wa Record Label ya Cheusi Dawa Fid Q ameweka bayana taratibu nzima za uachiaji wa albamu yake ya tatu “KitaaOlojia” yenye ngoma 20.

Mkali huyo wa Fresh na Fresh Remix Fid Q Kupitia kipindi cha The Splash cha Ebony FM amefunguka kwenye Pigia Mstari na Watangazaji Chris Bee na  Fredoo Mbunji, ambapo awali kupitia kipindi hicho aliahidi albamu tyake hiyo kutoka Agosti 13, ambayo pia ni tarehe yake ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.


“Ni kweli ngoma zimekuwa zikitoka nyingi unajua sio tu kuna Fresh kuna Ulimi Mbili,kuna albamu ambayo inatakiwa itoke nachoweza kusema itafuatia kwanza video ya Ulimi Mbili halafu kisha tutawatangazia tarehe ambayo tutaachia albamu” amesema Fid Q.


Fid Q ana albamu mbili kwenye soko la muziki. Albamu ya kwanza inaitwa inayoitwa "Vina Mwanzo Kati na Mwisho" na mwishoni mwa mwaka 2009 alitoa albamu ya pili “Propaganda”, ambayo imepokelewa vizuri sana Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki. 


Hata hivyo Mashabiki wa Hip Hop wanaichukulia “Propaganda”. kama ni albamu bora kabisa, yaani 'classic' huku akili na masikio yao wakielekeza kuingoja albamu hiyo mpya na ya tatu kutoka kwa Fid Q kama inaweza kuvunja rekodi ya albamu ya “Propaganda”.

Post a Comment

 
Top