Menu
 

Baada ya ukimya wa takribani miaka saba, wakundi la “Wakali Kwanza” sasa kaa mkao wa kula kwa coming back yao ya hatari iliyotayarishwa na timu nzima ya MJ Records, label ambayo awali ilikuwa ikiwa simamia.

Crew member wa Wakali Kwanza Makamua amekiambia kipindi cha The Splash cha Ebony FM wakati akipiga stori na Watangazaji wa kipindi hicho Chris Bee na Fredoo Mbunji, kuwa ni wakati wao sasa kuchukua nafasi kwenye Bongo Music Industry na kukata kiu ile ambayo mashabiki wameimiss kutoka kwao.

“Sio mbaya, Watu watapata product nzuri, watapata muziki mzuri wa dunia sisi tunaamini kuwa tutatetemesha dunia, dunia itatetema kwa hiyo kila kitu kitakuwa sawa” amesema Makamua kwa tambo.

Mara kadhaa wasanii wengi huwa hawasiti kutoa majingambo na kuwaaminisha mashabiki wao kuwapa burudani lakini wapo waliofanikiwa kukamilisha ahadi na wapo wale ambao kato hawajasikika tena kama walivyoahidi.

“Very soon! Unajua kila kitu nikujipanga sio tu kutoa records, rocord zipo lakini nini ambacho tumekiplan kwa ajili ya watu, nini kizuri watu wakione nini kizuri watu watakipenda kwa hiyo ni plan kubwa.

Hiyo ni kitu kikubwa ambacho kimetuumiza sana akili na inatuumiza sana akili sio sisi tu pekee yetu waimbaji na Menejimenti pia kwa ujumla” amesema Makamua.

Makamua amesema licha ya kutangaza kurudi kwenye game kwa Wakali Kwanza lakini kuna jambo muhimu ambalo walionelea ni vema kuliweka sawa ili kuimarisha ngome yao.

“Sio mbaya kwa sababu aaah kitu kikubwa ni kwamba ni muda mrefu tumekaa party kwa hiyo ile re-union tumeitengeneza na lazima sisi wote watatu tuwe na common interest, tushikane, tuambatane natujue nini tunafanya, as you can see tumekaa MJ Records for three years now nadhani sasa ndio muda mzuri waku speed out” ameongeza Makamua.

Post a Comment

 
Top