Menu
 


Novemba 17, 2016 ilikuwa ni tarehe rasmi ya mkali wa “Sina Hali” Timbulo kurejea katika Gemu la muziki wa kizazi kipya na ngoma adhimu iitwayo “Usisahau” akimshirikisha Barakah The Prince baada ya ukimya wa miaka miwili.Mpaka sasa Timbulo amekwisha kuachia jumla ya ngoma 5 ikiwemo Usisahau, Mfuasi, Ndotoni, Mshumaa na Sina Hali na tunaweza kutafsiri kuwa ni dalili za ujio wa albamu mpya ya msanii huyo?.


“Off course namshukuru Mungu nimekuwa nikitekeleza kweli ahadi kwa mashabiki, nafikiri nikutokana tu na wakati kila siku nasemaga hivyo kwamba time kama imekuwa nzuri kwangu mambo yamekuwa mazuri na Mungu anaendelea kubless kile ambacho alikiweka ndani mwangu, aaaah jambo la msingi na kubwa zaidi hiyo inaweza kuwa ishara ya albamu”


Amesikika Timbulo kwenye Pigia Mstari ya The Splash ya Redio Ebony FM wakati akihojiwa na watangazaji Chris Bee na Fredoo Mbunji.


“Albamu ndio kitu ambacho nimekuwa sasa hivi niseme kwamba kimekuwa bado kinaniumiza kichwa na kila nikilala nikiamka nawaza nawezaje kuileta albamu kwa mashabiki ambao wanapenda muziki wangu imebaki kuwa kizungumkuti kwa namna moja ama nyingine kwa sababu ni kitu well ambacho nakipigania natamani pia kuwa na heshima hiyo naamini muda si mrefu tutaweza kujua namna gani tunaweza kufanya” Ameongeza Timbulo.

Post a Comment

 
Top