Menu
 

Wakati Mashabiki wa Bongo Flava na muziki mzuri Tanzania wakiendelea kusubiria ujio wa ngoma mpya ya Msanii wao nguli Alikiba, baada ya kusambaa kwa tetesi kuwa huenda ingetoka Agosti 3 mwaka huu. Miongoni mwa mameneja wa Alikiba aitwae Aidan amepigia mstari kupitikia Kipindi cha The Splash cha Redio Ebony FM na Watangazaji Chris Bee na Fredoo Mbunji na kukiri kuwa ngoma hiyo mpya itatoka kuanzia sasa mpaka kufikiwa Agosti 31 mwaka huu.

"Basi ndani ya siku hizi 30, kutakuwa na update kuhusu kazi yake mpya, Alikiba tangu mwanzoni mwa mwaka amekuwa kwenye Tour alienda South Africa akakaa almost mwezi mzima na aliporudi hapa alifanya mapokezi wa Tuzo ile ya MTV EMA na kesho yake akaenda Tour Marekani" amesema Aidan.

Licha ya Msanii huyo kipenzi cha watu Alikiba akiwa busy na majukumu ya Ziara yake huko Ughaibuni, lakini suala hilo limeonekana si chochote kwa wadau na mashabiki wake na kubaki na msimamo wakumtaka aachie wimbo mpya.

"Amekuwa on Tour mara nyingi kwa hiyo anakosa muda wakuwepo nchini wakuweza kufanikisha vitu vingine viweze kuendelea, kwa sababu ni vizuri ukiwa unatoa wimbo uwepo mwenyewe kufanyia promotion na mambo mengine" amesema Aidan.

Aidha ameongeza sababu za kuendelea kuchelewa kuachia ngoma mpya "Kwa hiyo tangu ametoka Marekani amerudi,  ameenda Uingereza kwenye Show ile ya One Africa  Music Festival, ametoka ameenda Belgium amerudi sasa hivi ameenda Kenya kwenye Kampeni na ataenda tena New York  kwenye Tamasha la One Africa Music Festival atakaporudi kwa hiyo atakuwa na muda kidogo wakuachia ngoma na kuifanyia Promotion".

Post a Comment

 
Top