Menu
 

Starboy Wizkid anarejea tena nchini Marekani kufanya collabo na mwanadada Nicki Minaj, baada ya wiki mbili toka aliporejea nyumbani kwake nchini Nigeria. 


Mkali huyo hivi karibuni ameachia kanda mseto(mixtape) yake iitwayo Sounds From The Other Side(SFTOS), amekuwa mwenye mafanikio makubwa baada ya kuanza kupenya kwa kasi katika soko la muziki la nchini Marekani ambalo, linatafsiriwa kuwa ni gumu kwa msanii wa Afrika kupenya.

Wizkid anatarajia kusafiri hadi Atlanta USA kukamilisha mchongo huo wa collabo na Nicki Minaj sambamba na kuendelea na ziara yake ya kimuziki iitwayo Africa to the world campaign.

Collabo hii ilianza kutabiriwa baada kuonekana katika Club moja ya usiku Wizkid akikumbatiana kwa furaha na US Female Rapper Nicki Minaj

Tayari wote hao wawili kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii wameweza kupost na kushare picha ya pamoja kwa mashabiki wao wakiwa wameketi na kuelekezana jambo, wakiwa studio jambo ambalo limeashiria kuwa kuna collabo inafuata.

Mpaka sasa pia Wizkid amekamilisha collabo na Star mwingine kutoka marekani aitwae Future ambayo itatoka wakato wowote, hivyo yafaa kutafsiri kuwa collabo ya Nicki Minaj na Wizkid itakuwa pia ni njia moja wapo kwa Wizkid kuendelea kulipenya soko la muziki nchini Marekani.

Post a Comment

 
Top