Menu
 


Mara kadhaa kumekuwa na miong’ono, baada ya kusambaa kwa tetesi kuwa kuna ugomvi baina ya miamba miwili kwenye Bongo Music Industry na washikaji wakaribu Roma na Moni Centrozone. Rapper Roma(kushoto) na Moni Centrozone(kulia).

Kupitia The Splash ya Ebony FM, Rapper na Hitmaker wa Matango Pori amekanusha vikali kuhusu tuhuma hizo, wakati akihojiwa na watangazaji Chris Bee na Fredoo Mbunji.

“Mimi toka nafanya muziki sijawahi kuwa na bifu na mtu yeyote, labda mtu mwingine anaweza akawa na bifu na mimi, so huwaga sina matatizo na mtu nafanya kazi zango, naangalia maisha yangu na angalia muziki wangu unaenda wapi” amsema Moni.

“Sijawahi kuwa na bifu na mtu, labda mtu akaweka bifu na mimi au akawa na chuki zake binafsi na mimi kwa hiyo mimi niko fresh sina tatizo na mtu yeyote, sijajua kwa upande wao hao mnaowaongelea lakini mimi niko zangu fresh” ameongeza Moni.

Kwa upande mwingine Moni anafungukia kama yupo tayari kufanya ngoma nyingine na Roma ili kutudhihirishia kuwa hawana ugomvi.

“Kufanya collabo na mtu haimanishi kwamba ndo hamna bifu, mnaweza kufanya collabo na mna bifu na mnaweza msifanye collabo na mkawa piece, so kufanya collabo haimanishi kwamba labda ndo mnachukiana au una bifu na mtu na sio kama nikifanya collabo nyingine ndo zitadhihirisha sina bifu na mtu” amesema Moni.

Hata hivyo Moni Centrozone na Roma wameshawahi kufanya kazi mbili za pamoja kama “Usimsahau mchizi” na “Hatuhesabu Masaa”.

Tazama hapa Video Mpya wa Moni ft Barakah The Prince - Matango Pori.

Post a Comment

 
Top