Menu
  Rudeboy (Paul P-Square)
Mara kadhaa imekuwa ikisifika kuwa Miongoni mwa Mapacha waliokuwa wakiunda Kundi la Muziki la P Square lenye maskani yake Nchini Nigeria Rudeboy(Paul P-Square) kuwa ana kipaji kikubwa cha kuimba pekee, huku pacha mwenzake Mr. P (Peter P-Square) akisifika kuwa ana kipaji kikubwa cha kudance kuliko kuimba.


Sasa kaa humu…… Kumbe hata Rudeboy (Paul PSquare) ana kipaji kikubwa pia cha kudance na sikuimba pekee kama inavyodhaniwa, wengi wakiamini kuwa huenda kipaji chake cha kuimba ndicho humpa kiburi na kutochukua uamuzi wa kujifunza kucheza kama ilivyokuwa kwa mwenzake ambae amekuwa kivutio kikubwa kwa vijana na mshabiki wengi wanaopenda dance.


Sababu zinazomfanya Rudeboy (Paul P-Square) kutoonekana kujishughulisha katika kudance kwenye video na matamasha, imetokana na ajali ambayo aliwahi kuipata wakati wakifanya mazoezi kwa ajili ya tamasha moja yayopelekea mpaka sasa kuwa na maumivu akitaka kudance ambayo humfanya kushindwa kufanya hivyo. 


Pata picha isingekuwa maumivu hayo Rudeboy (Paul P-Square) tungemuweka katika nafasi ipi endapo vipaji vyote viwili vya kuimba na kudance angekuwa anavionesha kwa hadhira?

Post a Comment

 
Top