Menu
 Mkali wa Seduce Me na Mmiliki wa Recording Label ya King Music, Alikiba ameipaisha Bongo Flava ya kizazi cha sasa nakudai bado iko hai na wasanii vijana(chipukizi) wanaitendea haki na kuongeza chachu ya ushindani.

Alikiba ambaye ni miongoni mwa jopo la Wakurugenzi wa Music Label ya kimataifa iitwayo ROCKSTAR4000, imeipinga vikali dhana iliyotawala kuwa muziki wa Bongo Flava umetawaliwa na vijionjo vya Afrika Magharibi.

"Bongo Flava bado haijaharibika na bado inafanya vizuri, na hata ukiangalia kuna wanamuziki wengi, so much competition in Tanzania" amesema Alikiba.

Hata hivyo Alikiba hakuacha kuwapa pongezi wasanii wenzake wa Bongo Flava kwa harakati zakuupa thamani muziki huo.

"You can see kuna vijana wengine wadogo wanafanya vizuri na wanatuwakilisha so tunafurahi jinsi gani bongoflava inaweza kufanya vizuri kwa sababu East Africa muziki unaoongoza kwa kufanya vizuri" ameongeza Alikiba.

Post a Comment

 
Top