Menu
 Davido ni miongoni mwa Wanamuziki wenye mafanikio makubwa katika tasnia ya muziki barani Afrika, na safari hii ameamua kuvunja ukimya nakutoa ishara yakuwepo kwa ngoma ambayo amemshirikisha staa mkubwa na mwenye mafanikio Afrika Kusini Cassper Nyovest.

Kupitia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa Instagram, Davido ame-share na mashabiki wake kipande kifupi cha video akiwa studio na Cassper Nyovest pamoja na washikaji zao wakiisikiliza ngoma hiyo iliyopewa jina la Classic.

Cassper Nyovest na Davido wote wawili mwishoni mwa juma lililopita waliibuka washindi waktika Tuzo za Sound City MVP, ambapo Davido alijishindia Tuzo mbili za Wimbo bora wa Mwaka na Video bora ya mwaka kupitia ngoma yake ya FALL huku Cassper Nyovest aliibuka mshindi wa Tuzo ya Msanii Bora wa HipHop barani Afrika.

Post a Comment

 
Top