Menu
 Hitmaker wa Naumia Roho DULLAYO amekiri nyimbo zake kadhaa kumwendea mrama, na anachokifikiria kwa sasa kurejelea mfumo wa awali wa muziki uliomtambulisha.

DULLAYO amesema mfumo aliokuwa akiutumia awali ndio uliokuwa ukimfanya kuheshimika katika Music Industry nakukonga nyoyo za mashabiki.

''Kwa sababu ya matarajio yangu kutofikia mafanikio, kwa hiyo hivi soon nitaachia Video pamoja na audio ikiwa katika miondoko ya Rap, nitaachia mwezi huu inafanana na miondoko ya Naumia Roho so fans wangu wakae mkao wa kumeza kwani watamsikia DULLAYO yuleyule wa kwao wakipindi cha nyuma'' amesema Dullayo.

Kwa upande mwingine DULLAYO kama mzazi amemwelezea Mtoto wake SAMEEL kuwa huenda akaja kuwa mtu maarufu sana kutokana na dalili anazozionesha kupitia vitu anavyovipenda na anampa baraka zote za mafanikio.

''SAMEEL mtoto wangu namlea vizuri, mimi nafikiri mtoto wangu atakuwa star jinsi navyoona utundu wake nini licha ya kuwa ana umri mdogo lakini anapenda sana muziki, japo sipendi mwanangu ajekuwa mwanamuziki napenda asome awe msomi na elimu imkomboe na kuwa msaada mkubwa katika jamii na taifa kwa ujumla'' amesema Dullayo.

Post a Comment

 
Top