Menu
 MWAAH ni ngoma unayoendelea kujivinjari nayo kwa sasa kwenye Playlist ambao ni ngoma ya kwanda kutoka kundi linaloundwa na wasanii wawili wa Moni Cetrozone na Country Boy liitwalo MOCO.

Licha ya kitaani wengi wakihisi ni kundi rasmi kwenye Muziki wa Hiphop, Country Boy athibitisha kuwa MOCO sio kundi bali ni muunganiko tu.

"MOCO sio kundi as kundi official, MOCO ni muunganiko wa watu wawili ambo ni Moni na Country Boy tunapokuwa tunafanya kazi pamoja, kila project tunapokuwa tunafanya pamoja  ukimsikia Moni ukimsikia Country ndio unapata MOCO" amesema Country Boy.
  
"Sisi ni washikaji wa muda, tumekaa kwanza takribani kama mwaka mzima kuanza kusomana, kujuana kitabia, kwanza tumeanza kukaa pamoja sometimes tumeweza ku-hang up pamoja tujuane kabla ya kufanya kazi kwa tulikata kuanza kuwa sure  before yakuanza kufanya kazi" ameongeza Country Boy.

Moja ya njia waliyoitumia kusomana vema ni kupitia ushirikiano waliokuwa nao katika matamasha mbalimbali kama vile Fiesta nk.

"Tumeanza kuwa na chemistry muda mwingi sana na kazi pia tuimeanza kutengeneza mwaka uliopita mwishoni mwishoni tumefanya projects nyingi sana" amesisitiza Country Boy.

NEW VIDEO:- MOCO - MWAAAH 


Post a Comment

 
Top