Menu
 

Baada ya Kufanya vizuri na tamasha lake la Nyumbani liitwalo Home Sweet Home la Hitmaker wa "Baraka" Izzo Business, kwa misimu ziadi ya minne mfululizo mkali huyo aibua kubwa zaidi.
Rapper Izzo Business

Home Sweet Home ni msimu wa burudani ambao hufanyika Jijini Mbeya na Izzo B hutumia kama siku maalumu ya kujumuika na mashabiki wake kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake ambao hufanyika 25 Desemba kila mwaka kwenye sikukuu ya Kristmasi siku ambao pia wakristo duniani huadhimisha kumbukumbu yakuzaliwa kwa Mkombozi wao Yesu Kristo.

Habari njema kutoka kwa Izzo B ametangaza kwa mashabiki wake Tanzania nzima kuwa Tamasha la Home Sweet Home halitifanyika Mbeya tu pekee.

"Aaaah Sababu kubwa za kuongeza mikoa unajua kwa sababu muda mwingi imekuwa ikifanyikia Mbeya na si kwamba mashabiki wa Izzo wapo Mbeya tu au sio wako kwenye mikoa tofauti tofauti na hii ilikuwa ni kuvuta nguvu na kujipanga ili tamasha lizoeleke kwanza" amefunguka Izzo B.

Hata hivyo Izzo B ametudele kuwa anathamini mashabiki kila kona na hivyo ni wakati muafaka wakuwafikia kila sehemu walipo.

"Kwa hiyo imekuwa mimi mwenyewe nikisafiri baadhi ya mikoa wanaulizwa bwana huku unakuja lini unakuja lini? Kwa hiyo hopely mwaka huu Mungu akipenda tutaanza na sijajua sasa ni tukaanzia wapi kwa sababu bado tunatafakari lakini nafikiri kuanzia mwaka huu kila kitu kitakwenda sawa" amesema Izzo B.

Post a Comment

 
Top