Menu
 

 
Imeripotiwa kuwa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza klabu ya Chelsea wana muhitaji straika wa West Ham United Andy Carroll kwa mkopo.
 
Chelsea hawajafanikiwa kufunga goli katika michezo mitatu mfululizo na kuwa mara ya kwanza kwao kufanya hivyo katika historia ya klabu, pia Chelsea ndiyo timu yenye magoli machache kuliko zile timu saba za juu kwenye msimamo wa Ligi.

Kocha Antonio Conte anataka kuongezea nguvu safu yake ya ushambuliaji baada ya Alvaro Morata fomu yake kuzidi kuporomoka kwa siku za hivi karibuni, wakati Eden Hazard naye bado hayupo fiti. Conte bado hajaridhishwa na Mitchy Batshuayi kama mbadala wa Morata.

Ripoti imesema kwamba mapema mwezi huu Carroll anatolewa macho na mabingwa hao, na Telegraph limesema kwamba mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool anatarajiwa kuchukuliwa kwa mkopo.

Chelsea pia wanamfukizia Richmond Boakye kutoka Red Star Belgrade pia Christian Benteke wa Crystal Palace, pia matumaini yao ya kumnasa Alexis Sanchez kutoka Arsenal sasa yanazidi kudidimia.

Carroll ameanza mechi 3 tu msimu huu kwenye Ligi Kuu chini ya David Moyes na amefanikiwa kufunga magoli 2 kwenye mechi 14 katika mashindano yote msimu huu.

Post a Comment

 
Top