Menu
 Mwanamuziki mkongwe Ruta Maximilian Bushoke a.k.a Bushoke amekiri kutumia majina ya Kibantu katika nyimbo zake yamekuwa msaada mkubwa kwa muziki wake kupenya kitaani.

Bushoke ambaye kwa sasa anafanya vema kwenye gemu la muziki wa kizazi kipya na ngoma iitwayo Goma la Ukae, iliyotayarishwa na Producer Abby Dady kutoka Square muziki ameiambia The Splash ya Ebony FM inayotangazwa na Chris Bee na Fredoo Mbunji namna anavyoabudu majina ya kibantu.

"Ukae ni nyumbani ni kibantu kuna baadhi ya makabila mawili matatu yanatumia kwa hiyo siwezi kusema ni kizaramo au nini kwa sababu sio specific ni kizaramo pekee ake au labda kabila fulani pekee yake bali ni kibantu kiujumla kwamba Goma la Ukae ni goma la nyumbani au linalochezwa nyumbani" amesema Bushoke.

Hata hivyo ameeleza sababu za msingi zakufanya kazi na Producer Abby Dady.

 "Nilivyomchunguza ni mtu ambae anapiga piga sana ngoma kati ya maproducer ambao wamejaaliwa sana kwenye upande wa ngoma, anavyotengeneza beat Abby Dady yupo vizuri kuja na kitu cha pekee yake kwa hiyo niliona kwa sababu Goma la Ukae ni kitu cha utofauti basi nimpatie Abby Dady" amesema Abby Dady

Tazama Video Mpya ya BUSHOKE - GOMA LA UKAE.

Post a Comment

 
Top