Menu
 Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho yupo mbioni kuingia kandarasi mpya na timu hiyo itakayomfanya kusalia Old Trafford mpaka mwaka 2021.

Mourinho alijiunga na United katikati mwamsimu wa mwaka 2016 kwa mkataba wa miaka mitatu utakaomuweka hapo mpaka 2019  akichukua mikoba ya Louis van Gaal.

Inaaminika kuwa wakala wa Mourinho, Jorge Mendes ameanza kufanya vikao vya mkataba mpya na United tangu mwezi Oktoba mwaka jana.

Natoka kipindi hicho, Mourinho amefanya maamuzi yakuhitaji kusalia Old Trafford.

Hata hivyo ameongeza kuwa lengolake kubwa ni kuhakikisha anairudisha timu hiyo katika makali yake iliyokuwa nayo hapo hawali.

Post a Comment

 
Top