Menu
 Klabu yenye mashabiki lukuki Dunia Manchester United yenye masikani yake Nchini Uingereza imetenga kiasi cha fedha paundi milioni 25 ili kuweza kuinasa sahihi ya Winga raia wa Brazil Lucas Moura anayekipiga katika Klabu ya PSG ya Ufaransa.

Ikumbukwe Mwaka 2012 aliyekuwa Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson, alikuwa na mipango yakumnasa winga huyo lakini akakutana na kikwazo baada ya PSG kushushiwa rungu la adhabu ya kuzidisha kiwango cha matumizi ya fedha klabuni hapo kinyume na pesa wanazoingiza.

Lucas Moura mwenye umri wa miaka 25, amekuwa chaguo namba moja la Kocha wa Manchester United Jose Mourinho kutaka kumnasa kwa lengo la kuboresha kikosi chake.

Post a Comment

 
Top