Menu
 Wakati wadau na mashabiki wa muziki Afrika Mashariki wakisubiria kwa hamu performance kali ya Kundi bora la dance Ghetto Kids kutoka Uganda, kwenye jukwaa la Grammy Awards 2018 wakiwa sambamba na Rapper French Montana kupitia ngoma ya Unforgettable.

Habari njema ni kwamba Rapper kutoka Kenya Octopizzo amepata mualiko "Invitation" kuhudhuria kwenye event kubwa ya utoaji tuzo za Grammy Awards New York, USA.

Octopizo atawakilisha East Africa kwenye event hiyo itakayofanyika January 28. Na kupitia ukurasa wake kwenye Mtandao wa kijamii wa Instagram ameweza kushare taarifa njema kwa mashabiki wake.

Post a Comment

 
Top