Menu
 Rapper na Hitmaker wa Mbwa Koko Mr Blue awataja wahusika waliolengwa katika ngoma yake hiyo, ambayo imefanikiwa kupenya vema kitaani.

Yapo maswali kutoka kwa baadhi ya mashabiki wakijiulizwa amekutwa na jambo gani lililosababisha kuja na ngoma yenye maudhui yakudiss watu?

"Aaaah Mbwa Koko ni kweli wapo na wapo kila kona wapo mbwa wenyewe kabisa,mbwa ambao ni koko wapo binadamu ambao wanafanya mambo kama mbwa koko" amesema Mr Blue

Kupitia The Splash ya Redio Ebony FM, Mr Blue ameenda mbali kwa kutolea mfano baadhi ya watu hao wanaofanya mambo kama Mbwa Koko  wakati akihojiwa na Watangazaji Fredoo Mbunji na Chris Bee.

"Wapo wanawake pia ambao wanafanya mambo kama mbwa koko, wazuri lakini uzuri wao unaishia tu barabarani ukisema umuoe, umchukue au utakiwe umchumbie sio mwanamke wakusema ukae nae na kuna Ma MC pia ambao ni mbwa koko kwa hiyo mbwa koko wapo na hatuwezi kuwakimbia" amehitimisha Mr Blue.

Post a Comment

 
Top