Menu
 Hitmaker wa Sitaki Kuumizwa Sajna amesema kuwa muziki sio kuimba tu ila ni kutengeneza nyimbo ambazo zitakuwa zinadumu kwa kipindi kirefu kuanzia miezi sita na zaidi.

Ujumbe mzito wa mashairi ndio unaomata na wenye kutoa mafunzo ndani ya jamii na sio wenye kusababisha mmomonyoko wa maadili.

 “Hata mama yangu alishaniambia, dada yangu, kaka yangu umeona nyimbo za zamani za akina Mubaraka Mwishehe na mwengineo sio kwamba wamekufa ndio zinafanya vizuri hapana hata leo akisikiliza mtu fulani anapata ujumbe kutokana na kutengeneza wimbo wenye uhalisia" amesema Sajna.

"Huwa wananikumbusha kuwa unaiona Iveta yako ulivyoitengeneza ina uhai, Sitaki kuumizwa, Mganga ni wimbo ambao kila mtu akiusikiliza lazima imkumbushe kitu fulani” ameongeza Sajna.

Post a Comment

 
Top