Menu
 Hitmaker wa Bado Kidogo Ben Pol ameeleza msimamo wake, wakutaka kuona vijana wakifanikiwa nasio kukata tamaa na kuendelea kulalamikia hali ngumu ya maisha.

Ben Pol ametudele kuwa dundo la Bado kidogo lilikuwa zawadi kwa vijana wenzake kuitambua nafasi walizokuwa nazo kwenye jamii.

"Nimeutoa kuhamasisha vijana wenzangu na watu wote, watanzania wenzangu, wapambanaji wenzangu kukaza moyo licha ya changamoto mbalimbali zinazotokea kwenye maisha kukatishwa tamaa, kukosa nafasi kwa wakati mwingine mambo kuwa magumu wakati mwingine maisha kuwa magumu" amesema Ben Pol.

Hata hivyo Ben Pol amesema mtu yeyote anapokutana na ugumu ni matokeo yakufikia mafanikio.

 "Hakuna kukata tamaa nawaambia don't give up bado kidogo imebakiwa sehemu ndogo tu umeona hakuna kukata tamaa, kukata tamaa ni mwisho kabisa ni kitu ambacho ni option ya mwisho kabisa. Kwa hiyo najaribu kuongea na wenzangu kuwa hakuna kukata tamaa kwa sababu imebakia sehemu ndogo tu katika kazi, maisha, elimu nk" amesisitiza Ben Pol.

Post a Comment

 
Top