Menu
 Malkia wa Muziki wa Kizazi kipya Tanzania(BongoFlava) Lady Jaydee, aeleza namna atakavyonufaika na mkataba mpya aliosaini na Record Label ya Taurus Musik ya nchini Kenya. 

Ikumbukwe kuwa Mnamo Novemba 27, mwaka 2017 Taurus Musik iliingia makubaliano maalumu yakuwasimamia wasanii wawili akiwemo Lady Jaydee na Msanii mwenye asili ya Congo DRC Alicious.

"Mkataba mpya niliosaini niwa albums tatu, kila mwaka natakiwa kutoa albamu mmoja kwa hivyo na namna tunavyofanya kazi na hii Record label ni kitu tofauti na watu wengine ambao nimewahi kufanya kazi nao" amesema Lady Jaydee.

Mkali huyo wa Ngoma ya Baby Lady Jaydee, huku akiwa mwenyefuraha hajasita kuwajuza mashabiki wake namna atakavyonufaika zaidi na mkataba huo.

"Wana-invest pesa yao, wanaweka pesa kwenye kila kitu wanakulipia studio, wanakulipia audio tofauti na watu wengine ambapo unaweza kuwa unafanya nao kazi lakini inabidi wewe ndio u-invest utoe hela yako mfukoni" ameeleza Lady Jaydee.

"Na ninaona kwamba kitu ambacho kitaweza kutokea na hii record label mpya ni kwamba mtu hawezi akaweka pesa yake akakubali ipotee kwa hiyo watafanya kila njia kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha kwamba pesa yao inarudi wanapata faida na mimi napata faida" ameongeza Lady Jaydee.

Hata hivyo amemalizia kwa kueleza unafuu utakaokuwepo na kujivunia kuwepo chini ya Usimamizi wa Taurus Musik Record Label.

"Tofauti na ambavyo ilikuwa mimi naweka pesa yangu, kwa hiyo inabidi mimi ndio ni hustle hata kama mtu mwingine nafanya nae kazi lakini hawezi kusikia uchungu kwa sababu sio pesa yake hii ndio tufauti ya Record label mpya hii nayofanya nao kazi sasa hivi na watu wengine ambao nimewahi kufanya nao kazi hapo nyuma" amehitimisha Lady Jaydee.

Post a Comment

 
Top