Menu
 Kwa zaidi ya Miaka 7 kumekuwepo kwa Bifu kubwa ya maswahiba wa muda mrefu baina ya Wasanii wa Mduara baina ya Mfalme wa muziki huo AT na kundi la Offside Trick ambapo awali walikuwa wakifanya kazi pamoja.

AT ambae kwa sasa anafanya poa na ngoma yake iitwayo Kazi Yako, amekiri kujutia kuwajibu wasanii wa kundi la Offside Trick kupitia ngoma zake za Vifuu Tundu na Bao la kete kwa kuwa anahisi ndio chanzo cha kupotea kwao.

"Niseme ni kweli nilikuwa na Bifu na Offside Trick, aaah na mimi mwenyewe niseme kwamba yaani bora nisingewajibu, na ningeendelea kuimba kuliko kuwajibu kupotea kabisa kwa hiyo natamani uwepo wao wawepo lakini wafanye kazi zao kwaajili ya raia na sio kwaajili yangu mimi" amesema AT.

Pia AT amezungumzia mstakabali wa kufanya kazi na Offside Trick.

"Sijajua kama ipo siku nitafanya nao kazi kiukweli kwa sababu Offside Trick ambayo mi nimezinguana nayo sio hii iliyokuwepo kwa hiyo ni vitu vingine. Chochote kile kama raia wakiniruhusu huenda nikafanya nao kazi kwa sababu mashabiki wangu sitaki kuwa kera" amesema AT.

Hata hivyo AT ameongeza kwa kuzungumzia msaada ambao anaweza kuutoa kwa Offside Trick ili kurejea katika gemu.

"Kwa hiyo naweza kuwasaidia kuwaandikia lakini siwezi kuimba nao sauti ikawa pamoja na wao, lakini mashabiki wakisema hebu fanya kitu tuone mna-sound aje naweza kufanya nao ni washikaji ambao nimeweza kufanya nao kazi kwa muda mrefu" amesema AT.

Post a Comment

 
Top