Menu
 Tangu mwaka 2003 vinara wa ligi kuu ya EPL Manchester City hawajawahi kushinda katika uwanja wa Anfield, michezo 16 ya mashindano tofauti katika kipindi hicho City wameshindwa kupata alama 3.

Leo Man City wanakwenda kuitembelea Liverpool tena huku wakiwa wameshinda katika mzunguko wa kwanza lakini mara ya mwisho City kuwapiga Liva mara mbili katika msimu mmoja ilikuwa msimu wa 1936/1937.

Lakini msimu huo huo wa 1936/1937 ulikuwa msimu wa mwisho kwa Manchester City kuwafunga Liverpool zaidi ya mabao 3 katika mchezo mmoja jambk ambalo City alilifanha tena msimu huu alipowapiga Liva 5.

Ujio wa Virgil Van Djik unazidi kuwapa kiburi Liverpool kuelekea katika mchezo wa leo achilia mbali kwamba majogoo hao wa London hawajafungwa katika michezo yao 17 iliyopita na mara ya mwisho walipoteza vs Tottenham mwezi October.

Tangu msimu wa mwaka 1986/1987 hakuna timu ambayo imewahi kuwafunga Chelsea, Liverpool na Manchester United katika viwanja vyao vya nyumbani na kama leo Pep atawafunga Liverpool baasi atakuwa kocha wa kwanza kufanya hivyo tangu zama hizo.

Source:- ShafiihDauda

Post a Comment

 
Top