Menu
 Jina la Mshambuliaji wa Stoke City a.k.a STK Peter Crouch limejumuishwa na Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza Chelsea FC katika dirisha dogo lausajili baada ya Msambuliaji wa West Ham Andy Carroll aliyekuwa anawaniwa na mabingwa hao kupata majeraha.

Crouch mwenye umri wamiaka 36, alisaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kwenye Klabu yake mapema mwezi huu.

Lakini sasa ananyemelewa na Chelsea FC wakiangalia kikamilifu mshambuliaji mrefu kuchukua nafasi ya Michy Batshuayi ambaye ameshindwa kusaidiana na Alvaro Morata. 
 
Mchezaji wa West Ham Carroll mwenye umri wa miaka 29, kwa sasa amepatajeraha la mguu ambalo litamuweka nje ya Uwanja kwa muda wa wiki Nne hadi Sita .

Crouch ameichezea Stoke City mechi 186 na kufunga mabao 49 katika mashindano yote , ikiwa ni pamoja na matano msimu huu katika Kombe la Ligi. (The Telegraph )

Post a Comment

 
Top