Menu
 

 
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang amefikia makubaliano ya kujiunga na Arsenal uhamisho wa Januari kwa mujibu wa habari. 
 
Mustakabaliwa Aubameyang katika Westfalenstadion unazidi kuwa na sintofahamu kutokana na matatizo ya kinidhamu kuzidi kuongezeka msimu huu, baada ya kuachwa kwenye kikosi kilichoikabili Wolfsburg kufuatia kukosa mkutano wa timu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 sasa amekuwa kwenye rada za timu za Uingereza, na mwezi huu alikuwa akitajwa kuingia kwenye rada za klabu za China.

Hata hivyo, Express kimeripoti kuwa Aubameyang amefikia makubaliano na Arsenal kwa mkataba ambao utamfanya kuwa mchezaji anayelipwa dau nono zaidi katika historia ya klabu.

Uhamisho wake utategemea kuondoka kwa Alexis Sanchez mwezi huu, na mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile yupo mbioni kujiunga na Manchester United baada ya kufikia makubaliano na miamba hao wa Old Trafford.

Arsenal wameachwa pointi nane kuingia kwenye nafasi za kufuzu Ligi ya Mabingwa na wanataka kujiimarisha mbele kutokana na ukame wa magoli wa Alexandre Lacazette.

Licha ya matatizo yake dimbani, Aubameyang amefunga magoli 21 katika mechi 23 kwa Dortmund kwenye michuano yote.

Post a Comment

 
Top