Menu
 Kwenye Bongo Flava music industry unaendelea kujivinjari kuisikiliza na kuitazama "Mwanangu na Wanao" mradi mpya kutoka Kundi la Hiphop linalokuja kwa kasi OMG Tanzania wakiwa wamemshirikisha Female Rapper Rosa Ree.

Akifunguka kupitia The Splash ya redio Ebony FM, Salmin Swaggz crew mamber wa Kundi la OMG Tanzania, wamempa nafasi ya upendeleo Rosa Ree kusikika katika ngoma yao hiyo kutokana na nafasi yake ya juu uliyokuwa nayo kwenye Game kama kiongozi wa female rappers.

"Tumeamua kumshirikisha Rosa Ree kwenye ngoma yetu kwa sababu katika gemu ya sasa hivi, Rosa Ree ni msanii ambaye anaongoza kwa marapa wa kike tukasema Rosa Ree ni msanii mzuri na anaongoza sasa hivi na OMG ni miongoni mwa makundi ambayo yako mbele kabisa katika Hiphop sasa hivi katika muziki wa new generation tukasema tufanye nae kitu na pia tutatoa kitu kizuri" amesema Salmin Swaggz.

Aidha Salmin Swaggz amezungumzia namna wimbo wao wa Wanangu na Wanao ulivyotendewa haki baada yakufanikiwa kufikisha maudhui kwa jinsia zote mbili.

"Kama mtoto wa kike pia anawawakilisha watoto wa kike kwa sababu sisi Wanangu na wanao, tumeiimba kama wanaume  tume-represent wanetu wakiume kwa hiyo tukasema mtoto wa kike wakiwepo hapa nae atakuwa ana represent jinsia yake na watoto wa kike"amesema Salmin Swaggz.

Hata hivyo Kundi la OMG Tanzania linaundwa na vichwa vitatu ambavyo ni Young Lunya, Conboi na Salmin Swaggz.

Post a Comment

 
Top