Menu
 Kocha Arsene Wenger anaamini kuondoka kwa Alexis Sanchez hakutakuleta maumivu sana kama ilivyokuwa kwa Robin Van Persie alipoondoka mwaka 2012 na kujiunga na Man United.

Sanchez,29, anakaribia kujiunga na Man United baada ya kukataa kusaini mkataba mpya na Arsenal.

Sanchez anafanya alichofanya RVP mwaka 2012, ambapo aliweza kuisaidia Man United kuchukua ubingwa wa ligi kuu mwaka unaofuata.

" Tulimchukua Van Persie kipindi anacheza timu ya akiba ya Feyenoord " alisema Wenger jana Alhamisi.

 " Tulifanya kazi kubwa na yeye. Unapowafikisha wao pale na, baadaye wanaondoka, hiyo inauma sana ".
 
Henrikh Mkhitaryan anataraji kujiunga na Arsenal ikiwa ni sehemu ya dili hilo la Sanchez kwenda Old Trafford, na Wenger anaamini kuwasili kwa kiungo huyo wa Armenia kutapoza machungu ya kumpoteza Sanchez.

Post a Comment

 
Top