Menu
 Rapper Moni Centrozone.
Mkali wa Bongo Superstar Moni Centrozone licha yakuwa msomi wa Digrii ya Environment Disaster Management, aliyoichukua kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) amesema hafikirii katika maisha yake kuajiriwa katika taasisi yoyote ya Serikali au binafsi.

"Kuhusu suala la kuajiriwa hapana, siwezi kuajiriwa hata siku moja nitajiajiri mwenyewe Mzee" amefunguka Moni.

Huenda ikawa Moni Centrozone alipitia changamoto zakutafuta ajira zilizosababisha kuwa na fikra za kutokuajiriwa?

"Na suala la changamoto kufukuzia ajira hapana,sijawahi kufukuzia ajira sehemu yoyote changamoto ya ajira yangu niliyokutana nazo ni kwenye ajira yangu ya muziki ambayo nimejiajiri mwenyewe ndo changamoto nilizokutana nazo kwenye maisha yangu" amesema Moni.

Hata hivyo msanii huyo anayetokea kundi lisilo rasmi liitwalo MOCO ameongeza kuwa "Suala la ajira kufanya kazi sijawahi kwenda kutafuta kazi labda nilitumaga tumaga lakini sikufuatilia changamoto ila watu wananiadithia washikaji zangu wanakutana na changamoto sana ambazo zinawakatisha tamaa unajua ile so lakini mimi nimeamua kuendelea na sanaa kama ndo njia yangu".

Post a Comment

 
Top