Menu
 Baada ya mchezo wake wa Jana wa Ligi kuu Tanzania bara na kuibuka na ushindi wa goli 4 kwa 0 dhidi ya Singida United, kikosi cha wekundu wa msimbazi Simba SC kimewasili mjini Bukoba kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya Kagera unaotarajiwa kuchezwa january 22 (Jumatatu) kwenye Uwanja wa Kaitaba.

Kikosi cha Simba kimesafiri Alfajiri ya Leo kwa Ndege ya Air Tanzania na kuwasili mkoani Kagera na kuweka Kambi mkoani humo.

Akizungumza na wordsports14 manager wa Simba Richard Robert amesema kuwa baada ya mchezo wa jana walirejea Kambini na Leo wameelekea Bukoba kwa ajili ya Maandalizi ya Mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar. 

"Tunamshukuru mungu kwa ushindi wa goli 4 tulizozipata jana kwenye mchezo wetu dhidi ya Singida United na Leo Alfajiri tumesafiri na Air Tanzania kuja hapa Bukoba kwaajili ya maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar. Tunamshukuru mungu tumefika salama na tutafanya mazoezi baadae saa 10.45 Jioni" Richard

Simba imeendelea kutamba kileleni kwenye msimamo wa Ligi kuu Tanzania bara mara baada ya ushindi wa Goli 4 dhidi ya Singida United, na kuwa na pointi 29 Wakifuatiwa na wanalambalamba Azam FC wenye pointi 27.

Post a Comment

 
Top