Menu
 Rapper mwenye mfanikio makubwa kwenye Muziki wa Bongo Flava Joh Makini, alia na vipaji halisi vya wanamuziki kupotezwa na kutopewa kipaumbele ukilinganisha na ukubwa wa kazi zao wanazoziachia.

Kauli hii imekuja baada yakuibuka shutuma nyingi kuwa wasanii wenye vipaji kupotezwa na media sambamba na mashabiki kwa kutowapiga tafu na badala yake kuwapiga sana tafu wasanii wanaotengenezwa studio au ambao wanauwezo wakutumia pesa nyingi katika promosheni au kiki.

"Sitaki kusema kwamba kuna watu wengi wasiokuwa na vipaji kwenye gemu, lakini nitapenda kwa sababu naamini watu wote ambao wako kwenye vitengo husika,naomba hata akija mtu mabo unaone huyu ni real deal wanajua kwa hiyo tujitahidi kadri ya uwezo wetu kuwapa nafasi watu ambao tunaona kabisa huyu kweli ndie"amesema Joh Makini,

"Piga ua biashara zifanyike na kila kitu lakini tusipoteze talent yaani tusiache mtu yeyote mwenye kipaji yaani ukimuona mtu mwenye kipaji popote ulipo, make sure unafanya kitu kwaajili yake kwa sababu ni kitu pekee ambacho kimetuweka mimi wewe yaani sisi wote, tukiacha kwa mfano watu wenye vipaji vya kweli au watu wanaofanya vizuri kwenye muziki kwa maslahi yetu for example kukata tawi la mtu ambalo wote tumekalia" amesisitiza Joh Makini.

Kwa sasa Joh Makini anatamba vilivyo na ngoma yake iitwayo Mipaka.

Post a Comment

 
Top