Menu
 Mkali wa RnB Tanzania Rama Dee awashauri wasanii wenzake kuazingatia maadili katika ubatizaji wa majina ya nyimbo zao.

Rama Dee ambaye ambaye amefanikiwa kufungua mwaka 2018, kwa kuachia ngoma mpya iitwayo Furaha Yetu, akimshirikisha Joh Makini ameeleza ambacho huzingatia kabla ya kuibatiza jina ngoma yake.

"Nimeamua kuwa na majina tofauti tofauti kwa sababu natafuta majina ambayo yanaweza kuendana na watu ambao wanasikiliza muziki wangu, umeelewa kwa hiyo siwezi kusema natoa wimbo unaitwa Kifua halafu hauna maana yeyote" amesema Rama Dee.

Rama Dee hakusita kuwapa somo halisi wasanii ambao wamekuwa wakihisi kutumia jina lenye utata kwenye ngoma, inaweza kuongeza hamasa kwa mashabiki kuifurahia na kuipa nguvu.

"Lazima utoe wimbo ambao unaendana na mazingira ya watu ambao wananisikiliza mimi, kwa mfano Kuwa na subira, eeeeh Usihofia Wachaga, eeeeeh Sio waoaji hao, eeeeh Furaha yetu mpaka kufikia hapa nibebe na kila kitu natoa wimbo ambao unaendana na mazingira aaaah mimi naandika au naishi" amefunguka Rama Dee.

Post a Comment

 
Top