Menu
 


Rapper INSPECTOR HAROUN amedai Wasanii wakongwe hawashindwi kubuni mbinu mpya za kiushindani katika muziki na badala yake wanafanya muziki unaoishi hali inayowafanya washindwe kuwa na utaratibu wa kuachia ngoma mara kwa mara."Ukiwa kimya mashabiki wanahisi umeishiwa, sisi hatutaki kutengeneza muziki wa Big G, sisi tunatengeneza muziki unaoishi hatutengenezi muziki wetu kwa siku moja au mwezi mmoja au kila baada ya nusu mwezi kuachia ngoma. Muziki unaoishi unatakiwa uutengeneze ndani ya miezi kadhaa halafu maproducer tofauti tofauti wanakaa na kufanya kitu kizuri". amesema Inspector Haroun.Akiendelea na utetezi wa kauli yake Hitmaker huyo wa Pamba Nyepesi Inspector Haroun amesema "Kuna kitu ambacho mashabiki wa muziki kwa sasa wanakimiss, sawa wadogo zetu wanafanya vizuri, wanaimba vizuri wapo wengi wananyakua Tuzo na wengine wanaishia kuwa nominated lakini hawana uhalisia ukimsikia msanii huyu anafanana na msanii fulani unashindwa kuwatofautisha".Inspector Haroun anatoa ushauri upi kwa wasanii wa sasa? "Kikubwa wasanii walioingia katika gemu ni kuzingatia identity yao, uwepo wao wautambue unatakiwa kuwa kama wewe, wakati unapoanza muziki lazima utadokoadokoa sehemu ili upate njia yako ukishapata unatengeneza mfumo ya kujulikana kama wewe ndio maana sasa hivi AY, Juma Nature, Prof J, Afande Sele, Jay Moe na wengineo wanajulikana kama wao".


Post a Comment

 
Top