Menu
 

Beki wa Chelsea Andreas Christensen amejikuta kwenye wakati mgumu kutoka kwa wachambuzi wa soka na mashabiki wa Chelsea baada ya kutoa "boko" lililowagharimu Chelsea goli moja lililowapa sare Barcelona.

Ikiwa wapo mbele ya goli moja lililofungwa na Willian, Ilionekana The Blues wanaondoka na ushindi na faida ya goli moja kabla ya Mdenmark huyo kutoa pasi "isiyo na macho" eneo la hatari la Chelsea, pasi iliyomkuta mkongwe Iniesta aliyemtengea Messi aliyeingia kambani dakika ya 75.

Alipoulizwa Conte kuhusu boko alilolitoa Christensen amesema "Nafikiri uchezaji wa Christensen ulikuwa ni mzuri sana, kiwango kizuri. Tunamzungumzia mchezaji ambaye ana miaka 21 tu hapa.

Ni vigumu sana kumchagua mchezaji mmoja au mwingine lakini nafikiri Christensen alicheza mchezo wa kiwango cha juu. Niliridhishwa na kiwango chake.

Alikuwa ni moja wachezaji bora usiku huu (usiku wa kuamkia leo)".
 
Muitaliano huyo akaongezea kwa kusema "Nafikiri tulikuwa karibu sana kucheza mchezo kamilifu. Nadhani tulilipa kwa kosa moja. Lakini kama unavyojua vizuri, dhidi ya mchezaji wa aina hii kama Iniesta, kama Messi, kama Suarez ukifanya kosa unalipa". 

Chelsea sasa wanarudisha mawazo yao EPL Jumapili hii wakikipiga na Man Utd ndani ya Old Trafford huku Barca wakikipiga dhidi ya Girona Jumamosi hii, Mechi ya marudiano inapigwa tarehe 14 March ndani ya Camp Nou.

Post a Comment

 
Top