Menu
 Msanii wa kizazi kipya bongo Bakari Abdul maarufu kama Beka Flavour ameongea na kuweka wazi sababu kubwa iliyomfanya asihudhurie katika party ya kutambulishwa kwa aliyekuwa mwanamuziki mwenzie waliokuwa wakifanya kazi pamoja katika kundi la ya moto band kabla kundi hilo halijavunjika Maromboso.

Beka anasema sababu kubwa ni kucheleshwa kwa kadi ya mwaliko wa party hiyo, ambapo  siku analetewa kadi ya mwaliko hakuwepo nyumbani alikuwa anashoot video yake mpya, hivyo amerudi ndipo anakutana na kadi na kushindwa kujiandaa kwa muda huo.
"Taarifa niliipata lakini kadi nilicheleshwa kuipata, na ndio ikawa siku anatambulishwa na mimi niko location ya wimbo wangu mpya.nafika nyumbani usiku  nakutana na kadi  yaani ni usiku kwa usiku.kwaio mimi sikuweza kuwahi na kwenda lakini meneja wangu alituwakilisha" amesema Beka.
Hata hivyo Beka anasema kuwa anaamini kabisa kuwa Mboso ni msanii mzuri na ana lengo la kuifisha sanaa ya bongo fleva mbali hivyo nawaomba mashabiki wake wampe sapoti kubwa ili aweze kufanya vizuri.

Mboso na Beka wote walikuwa katika kundi la ya moto kabla halijavunjika , baada ya kuvunjika kila mtu alianza kutafuta ustaarabu wake na kutoka kivyake.hata hivyo wikiendi iliyopita Mboso alikaribishwa rasmi katika lebel kubwa nchini  ya WCB, huku ikitegemewa kuwa wasanii wenzie alikuwa akifanya nao kazi wangeweza kujitokeza kwenye jambo hilo la furaha lakini hali haikuwa kama ilivyo.

Wasanii wengine waliokuwa wakiunda kundi la ya moto kabla ya kuvunjika ni pamoja na aslay na Enock Bella ambao nao pia hawakufika .

Post a Comment

 
Top