Menu
 


Kiungo Mbrazil, Philippe Coutinho akiruka juu kushangilia baada ya kuifungia Barcelona bao la kwanza dakika ya 49 Uwanja wa Mestalla mjini Valencia.

Coutinho aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Andre Gomes katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Kombe la Mfalme. 

Hilo ni bao la kwanza kwa Coutinho tangu asajiliwe mwezi uliopita kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 145 kutoka Liverpool wakati bao la pili lilifungwa na Ivan Rakitic dakika ya 82 na wote walifunga kwa pasi za Luis Suarez. 

"Najisikia furaha sana kufunga Goli langu la kwanza Barcelona na kuweza kuisaidia timu kwenda Fainali"amesema Coutinho.
Barca inaingia fainali kwa ushindi wa jumla wa 3-0 baada ya Februari 1 kushinda 1-0 Camp Nou bao la Suarez pasi ya Lionel Messi dakika ya 67 na sasa itakutana na Sevilla iliyotoa Leganes kwa jumla ya mabao 3-1, sare ya 1-1 ugenini na ushindi wa 2-0 nyumbani.

Tazama picha zaidi hapa Chini.
 Coutinho akifurahia goli lake la kwanza Barca
 Messi akifurahi na kumpongeza Coutinho.
 Coutinho akimshukuru Mola baada ya kuifungia Barca goli la kwanza.
 Wachezaji wa Barca wakifurahia kwa pamoja goli la kwanza na Coutinho klabuni hapo.

Post a Comment

 
Top