Menu
 Mwanamuziki Nguli kutokea +234 Nigeria David Adedeji Adeleke a.k.a Davido amepokea Diamond Plaque na Platinum Plaque kutokana na mauzo mazuri ya kazi zake mbili za IF na Fall.

Kwa mujibu wa chama cha muziki nchini Afrika Kusini (RISA), Platinum ni 20,000 Units na Diamond ni 200,000 units.

Mbali na mauzo mazuri, Hits hizo alizotoa mwaka jana ziliweza kushika #No1 kwa wiki 9 mfululizo kwenye Radio.

Kwa sasa Davido anafanya vizuri na Hits za Fia na "Flora My Flawa", pengine na mwaka huu ukaenda kuwa mzuri kwake kutokana na kasi aliyoanza nayo.


 Davido yupo nchini Uingereza kwaajili ya tour yake ambapo wikiendi alitumbuiza jijini London kwenye ukumbi wa 02 Academy unaojaza watu 5000 (elfu 5)

Post a Comment

 
Top