Menu
 


Rapper King Crazy GK amesema ni busara kwa wasanii wa Bongo Flava kutangaza vivutio vilivyopo Tanzania katika video zao badala ya kutangaza mazingira na vivutio vya mataifa mengine.

Kupitia kipindi cha The Splash kinachosikika kupitia Redio Ebony FM GK amesikika akisema kuwa “Tanzania kuna vitu vingi sana vya kustajabisha,ambavyo mara chache unaweza kuvipata nje kuna Mlima Kilimanjaro kuna vitu vya akina Mkwawa kuna vituvingi ambavyo ukivionyesha dunia ina wonder”

GK ameongeza kuwa “Mzuri pesa umeiona nilimchukua Director wenye exposure nikashoot katika location ambazo wanazitumia wanamuziki wa kawaida hapa Tanzania lakini nilivyozitumia kila Mtanzania ameshangaa,Tuitambulishe zaidi Tanzania kimataifa tayari wenzetu South Africa wameshajitangaza tunaongezea kuwatangaza”.

Kwa hatua nyinine amesema ni wakati muafanya wa kuiendeleza Record Label ya EAST COAST TEAM kwa sababu ashasoma alama za nyakati muziki wa sasa unataka nini.

“Ni label kama zilivyo Label nyingine kubwa Afrika kama ilivyo Marvin kwa Nigeria ya Dony Jazzy imetengeneza wanamuziki wengi kama Tiwa Savage ni label ambayo inatengeneza wanamuziki kama GK alivyotengeneza akina AY, Mwana FA, O-Ten, TID, East Coast Team sio kwamba ilikuwepo na ipo kwa hiyo sasa hivi inaendeleza kuna wanaoingia watatengenezwa Mastar wengine wataachiwa  ni process sio kitu cha kusema asubuhi kesho tunakuwa pia kuna project nyingi zina kuja za GK na AY na Mwana FA.

Post a Comment

 
Top