Menu
 Mwanamuziki tishio kwa sasa kutoka +256 Uganda Spice Diana alazimika kuahirisha kufanya tamasha lake lililotakiwa kufanyika Februari 2 mwaka huu(leo), kufuatia kifo cha mwanamuziki kutokea kundi la GoodLyfe Radio kilichotokea jana Februari 1 mwaka huu.

Spice Diana ambaye amebahatika kushirikishwa na kundi la GoodLyfe(Radio na Weasel) kupitia dundo liitwalo Kyuma(chuma), ameutumia ukurasa wake wa facebook kueleza namna ukaribu wake ulivyokuwa na Radio sambamba na kutoa taarifa kwa mashabiki zake za kutofanya tamasha hilo.

"Nayakumbuka maneno uliyoniambia kuwa Spice huu ni wako(wangu) na ukaniahidi kuniandikia nyimbo 4 kwa mwaka huu, surprise ambayo ulinitengenezea mbele ya watu waliojitokeza kwenye sherehe yangu ya kuhitimu chuo, na ukanitakia mafanikio mema, Wewe ni mwalimu kwangu, mtu uliyenivutia kuwa mwanamuziki na rafiki yangu mkubwa"amesema Spice Diana.

"Kwa majonzi haya mimi na Uongozi wangu tumelazimika kusitisha kufanya tamasha iliyokuwa ifanyike Februari 2 mwaka huu(Ijumaa), hivyo tutatangaza tarehe mpya yakufanyika kwa tamasha hili hapo baadae baada ya kumpumzisha kaka yetu naamini mashabiki wangu mtaelewa na mwenyezi Mungu atupe wepesi katika kipindi hiki kigumu na ampumzishe kwa amani Kaka Radio" ameongeza Spice Diana.

.

Post a Comment

 
Top