Menu
 The Bongoflava Legend Dully Skyes, amefunguka kuwa yeye ndie msanii bora wa muda wote na anachukizwa na vitendo  vya kiki na matumizi ya dawa za kulevya.

“Kila kitu kuanzia uvaaji, kunyoa vile nilivyo naonekana kama wa leo, hata muziki wangu naimba wa kileo, siimbi tena muziki wa kizamani, kwa sababu zamani tulikuwa tunafanya muziki mzuri, sauti nzuri, beat nzuri, na vile unavyofanya show vizuri lakini siku hizi Kiki imekuwa ndio kila kitu ila mimi siwezi kwenda na Kiki nitafanya muziki tu ili mradi nijulikane mimi kama mimikwanza umri wangu umekwenda kwa hiyo nikitaka kufanya kitu kama Kiki vitaniangusha” 

Amepigia Mstari Dully Sykes a.k.a Babydee kupitia kipindi cha The Splash kinachoruka kupitia Redio Ebony FM.

Kwa hatua nyingine ameelezea kusikitishwa na wasanii kuendelea kutumia dawa za kulevya licha ya kuwa wqanajua kuwa yanaathiri maendeleo ya kimuziki, afya na akili.

“Kiukweli wasanii wengi wa zamani na wapo wasanii tunao madawa ya kulevya yamewaharibu kabisa katika vichwa vyao, wasanii wazamani watu wazima lakini bado wanaendelea na madawa wanaongea ovyo ovyo wanaropoka kwaajili ya dawa wanakuwa wanaharibika wanashindwa kufanya vizuri” amesema Dully Sykes.

Dully Sykes ameongeza kuwa yeye hawezi kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya kwakuwa ana familia.

“Mimi napambana kwa sababu nina familia, na watoto zangu, wadogo zangu na nina mama angu, wote wananiangalia sasa nikitaka kuingia sitokuwa mtu tena nitakuwa balaa, familia yangu itaishi vipi sasa mtu kama hutakuwa na majukumu basi unaweza kufanya vitu vya kipumbavu”.

Post a Comment

 
Top