Menu
 Licha ya mwanamuziki Mr Blue kufanya vizuri kwenye Bongoflava kwa muda wote toka alivyoingia kwenye muziki lakini ataja mapungufu yake.

Hitmaker huyo wa "Mbwa Koko" ameweza kushare mapungufu yake hayo kwa mashabiki wake wakati akizungumza katika The Splash ya redio Ebony FM akihojiwa na watangazaji Chris Bee na Fredoo.

"Kiukweli siri ya mafanikio ya uandishi wangu toka nianze game nikuangalia sana suala la ubunifu.....aaaaah naangalia sana ubunifu naangalia nini wanataka watu naangalia sana ideas" amesema Mr Blue.

"Mimi kwenye kuandika nyimbo kidogo sio mgumu sana lakini kwenye kutafuta idea ni mgumu sana huwa naangalia sana idea yakuandikia nyimbo" ameongeza Mr Blue.

Post a Comment

 
Top