Menu
 
Mwanamuziki Moses Ssekibogo ambaye jina la kisanii Mowzey Radio mwenye umri wa miaka 33, kutoka Nchini Uganda amefariki dunia asubuhi yakuamkia leo.


Radio ni miongoni mwa wasanii wanaounda kundi la GoodLyfe akiwa na msanii mwenzake Weasel ambae ni mdogo wake Jose Chameleone.


Umauti umemkuta Radio kufuatia kuvamiwa na kujeruhiwa kichwani na kuvunjika fuvu na uti wa mgongo baada ya kuanguka akiwa Bar maeneo ya Entebbe wiki mbili zilizopita nakupelekea kufanyiwa oparesheni ya ubongo katika Hospitali ya Case jijini Kampala kabla ya kuhamishwa kutoka Hospitali ya Mulago.


Katika jitihada za kunusuru uhai wake Rais wa Uganda Yowel Museveni alichangia kiasi cha shilingi milioni 30 kwaajili yakusaidia matibabu.Safari yake ya Muziki ilianza kwa kuwa backing vocal wa Mwanamuziki nguli nchini Uganda Jose Chameleone akishirikiana na msanii wenzake Weasel ambapo baadae mwaka 2008 waliondoka chini ya Usimamizi wa Jose Chameleone, kupitia kampuni yake ya Leone Island Crew nakuanzisha kundi la Goodlyfe.


Baada yakuanzisha kundi lao la GoodLyfe, Radio na Weasel walifanikiwa kupenya katikavituombalimbali vya redio na kitaani kupitia dundo lao la kwanza liitwayo Nakudata walioiachia mwaka 2008.


Tunachukua nafasi hii kuwapa pole ndugu, jamaa, marafiki na mashabiki na mwenyezi Mungu awape wepesi katika kipindi hiki Kigumu.


Imeandikwa na Chris Bee.

Post a Comment

 
Top