Menu
 Mkali wa dundo la "Love On The Brain" Robyn Rihanna Fenty a.k.a Rihanna anategemewa kuhudhuria mkutano mkubwa nchini Senegal, lakini vikundi vya dini nchini humo wamekataa kumpokea.

"Tumeukataa Ufreemason na mapenzi ya jinsia moja", shirika la vikundi 30 vya kidini wamesema, wakimshutumu muimbaji huyo kwa kutumia ishara za mazo na kuwa mjumbe wa chimbuko la Illuminati, lilanoaminika kuwa ni kundi maalum la watu ambao hudhibiti masuala na uongozi wa dunia na inasadikika kuwa hufanya shughuli zao kisiri kudhibiti kila kitu na kuunda Utawala Mpya wa Dunia.

Shutuma hizo zimefutiliwa mbali na wasanii waliowahi kufanya nao kazi huko nyuma, Rihanna atatembelea nchi hiyo ya Afrika Magharibi akiwa katika nyadhifa yake ya balozi wa shirika la elimu 'Global Partnership Foundation'

Shirika hilo lina maadhui wa kuchangisha fedha za kuwafundishia mamilioni ya watoto na vijana katika nchi zinazoendelea.

Chombo cha habari cha Jeune Afrique kimemnukuu Waziri wa Mambo ya Ndani akisema kuwa atahakikishia usalama washirika wote wa mkutano huo.

Post a Comment

 
Top