Menu
 Mkali wa dundo la "Niwe Dawa" Nini amefunguka kuwa hapendwi kuulizwa kama ana mahusiano ya kimapenzi na mtu gani kwa sababu ni maisha yake binafsi.

Kauli hiyo ameitoa kupitia The Splash ya Ebony FM wakati akihojiwa na Watangazaji Chris Bee na Fredoo Mbunji, baada yakupewa fursa yakuzungumza ni kitu gani ambacho hapendi kuulizwa?.

"Mmmmh kitu ambacho sipendi kuulizwa ni kama nini boyfriend ama sina" amesema Nini ambaye amekuwa akidaiwa kuwa na mahusiano na Msanii mwenzake Mr Nay a.k.a Ney wa Mitego Boss wa Freenation Records.

Lakini ni sababu zipi zinazomchukiza pindi akiulizwa swali hilo, masanii huyo ambae awali ndoa yake ya mkataba wa kikazi ilivunjika na Recording Label ya MJ records.

"Am sipendi kuulizwa hivyo kwa sababu sijui napenda tu watu wa-concetrate zaidi kwenye kazi kuliko kwenye mambo ya mahusiano, kwa sababu watu wanakuwa wana-concetrate zaidi kwenye mahusiano halafu wanakuwa wanasahau kuwa huyo mtu ana kazi ambazo wanatakiwa wa-concetrate zaidi, kwa hiyo ni suala ambalo sipendi kuulizwa kuwa una boyfriend au unatembea na mtu fulani, sipendi kwa kweli" amesisitiza Nini.

Post a Comment

 
Top