Menu
 


Hitmaker wa "Moyo Niache" Snura amezifungukia tetesi zilizozagaa kuwa anatoka kimapenzi na mkali wa "Seduce Me" Alikiba.


“Jamani mimi tena mahusiano na Alikiba ha ha ha haaaa…… Hee hizi stori zimetoka wapi jamani mbona kama mmeni-surprise mpaka mimi mwenyewe sasa….kiukweli hii stori mmeni-surprise sana” Snura ameidele The Splash ya Ebony FM akihojiwa na watangazaji Chris Bee na Fredoo Mbunji.


Snura ameendelea kukanusha vikali tetesi hizo nakuwataka mashabiki zake kuamini ukweli huu ambao umeuweka wazi.


“Alikiba ni mshikaji wangu tu ambae tumezoeana naye muda mrefu miaka mingi sana, Aaaaah tumezoeana hivyo ni washikaji ni watu ambao labda tumekutana ile tumeongea kawaida kishikaji kirafiki basi hakuna kingine chochote” amesema Snura.

Post a Comment

 
Top