Menu
 

  

HUKU Ligi Kuu barani Ulaya zikiendelea, tayari baadhi ya wachezaji wameonyesha uwezo wao mkubwa kutokana na namna wanavyozisaidia timu zao.

Hapa ni makinda 20 Bora ambao wana umri chini ya miaka 22 (U-22) wanaotisha katika Ligi Kuu Bora tano Ulaya.

Nyota wa Ligi Kuu England kama wa Swansea City, Tammy Abraham, beki wa Liverpool, Joe Gomez na wa Leicester City, Ben Chilwell, wote wamo katika orodha hii ambayo unaweza kuwaona hapa... 

8. Davinson Sanchez- Tottenham- (Thamani Pauni Mil. 58.6)Ameonekana sahihi moja kwa moja katika kikosi cha  Mauricio Pochettino kutokana na Mcolombia huyo kufiti mfumo wa mabeki watatu anaoupendelea kocha huyo. 

Alinunuliwa kutoka Ajax majira ya joto kwa pauni milioni 42, na tayari mchezaji huyo anaonekana kuwa biashara nzuri. 

7. Christian Pulisic- Dortmund (Thamani Pauni Mil. 66.5)Mzaliwa huyu wa Marekani ana rekodi nyingi kufuatia kuchomoza katika soka akiwa na umri mdogo. 

Ni kinda mdogo zaidi kuwahi kufunga katika Bundesliga, akiwa na miaka 19, winga huyo wasifu wake ulikubalika zaidi BVB.

6. Timo Werner -RB Leipzig (Thamani Pauni Mil. 81.8)Anatarajiwa kuiongoza Ujerumani katika michuano ya Kombe la Dunia majira ya joto nchini Urusi, Timo Werner tayari ana mabao saba katika mechi 10 za kimataifa alizocheza na bado anaonyesha uwezo katika Bundesliga akiwa na Red Bull Leipzig, ambayo ilimsajili kwa euro milioni 10 akitokea Stuttgart misimu miwili iliyopita.

5. Gabriel Jesus- Man City (Thamani Pauni Mil. 95.8)Kwa mujibu wa ripoti ya mtandao CIES, straika huyu Mbrazil, thamani yake imeongezeka zaidi ya mara mbili, tangu kuanza kwa msimu huu, kutokana na majukumu makubwa Jesus anayoyabeba na kuipa timu hiyo ushindi.

4. Marcus Rashford-Man United (Thamani Pauni Mil. 103.1)Ni tofauti kabisa kama alivyokuwa miaka miwili iliyopita. Marcus Rashford, wakati akipewa nafasi chache za kucheza, lakini kwa sasa anabaki kuwa mchezaji muhimu kwa klabu na nchi yake. Kwa sasa anaelezwa kuwa atakuwa mmoja wa washambuliaji bora duniani akiwa Old Trafford.

3. Ousmane Dembele-Barca (Thamani Pauni Mil. 106.4)Thamani yake inaeleweka ilishuka tangu kuanza kwa msimu, kufuatiwa na majeraha wiki moja tu akiwa Barcelona, lakini mrithi huyu wa Neymar-anabaki kuwa mmoja wa makinda bora Ulaya.

2. Dele Alli- Tottenham (Thamani Pauni Mil. 159.3)Mchezaji mwingine aliyeibuka misimu michache iliyopita, Nyota huyu wa kimataifa wa England, Alli, alisajiliwa na Spurs kwa pauni milioni tano tu na ana uwezo wa kuwa mmoja wa washambuliaji waliokamilika duniani, hususan wakati huu ambao tayari Real Madrid inavutiwa naye.

1. Kylian Mbappe- PSG (Thamani Pauni Mil. 161.6)Kinda aliyechomoza zaidi msimu uliopita barani Ulaya akitwaa ubingwa wa Ligue 1, na kisha kuhamia PSG baada ya miamba hiyo ya Paris kuridhia kumsajili kwa mkopo kwa makubaliano ya kumnunua jumla kwa euro milioni 180.

WENGINE WANAOINGIA KATIKA 13 BORA NI;
10. Theo Hernandez (Real Madrid) - Pauni Mil. 37.811. Youri Tielemans (Monaco) - Pauni Mil. 40.812. Federico Chiesa (Fiorentina) - Pauni Mil. 46.513. Gianluigi Donnarumma (AC Milan) - Pauni Mil. 49.2

Post a Comment

 
Top