Menu
 Msanii wa muziki kutoka Nigeria, Wizkid ameingia makubaliano ya kibiashara na kampuni ya Nike ambayo inajihusisha na utengenezaji wa vifaa vya michezo.

 Wizkid atahusika katika kutangaza jezi za timu ya taifa ya Nigeria ambazo zimetengezwa na kampuni ya Nike kwa ajili ya michuano ya kombe la duniani ambayo inatarajiwa kufanyika mwakani nchini Urusi.

“Joined Nike to Unveil the new Official Nigerian Jersey for the World cup, Russia 2018! Good luck to our players!! We got some more exciting news! Nike x Wizkid ๐Ÿ‘€ #NewFamily ,” ameandika Wizkid katika Instagram yake.

 Pia huenda kampuni ya Nike ikatoa bidhaa zake kwa wasio wanamichezo kupitia brand ya Wizkid.


Makampuni yanayojihusisha na utengenezaji wa vifaa vya michezo pia yamekuwa yakiwekeza katika wasanii ili kuweza kutanua wigo wa kibiashara.

Mwaka 2016 rapper wa Marekani Kanye West baada ya kufanya vizuri na brand yake ya Yeezy alipata dili la kampuni ya Adidas ambayo nayo pia inajihusisha na utengenezaji wa vifaa vya michezo.

Post a Comment

 
Top